Tovuti ya Lugha ya Alama

Furaha ya Viziwi kumjua Mungu

Njia gani waliyoipata viziwi kumjua MUNGU?

Kwa kutumia Lugha ya alama hasa DVD Biblia ya Lugha ya alama viziwi wengi wameweza kuelewa na kujua neno la Mungu. Pamekuwa na ushuhuda mwingi toka kwa viziwi kuhusu walivyokuwa wakipata shida wakiwa kanisani. Wanaeleza kuwa mara nyingi walikuwa wakifuatana na familia zao kwenda kanisani na wakifika huko walikuwa hawaelewi chochote kilichokuwa kikiendelea hapo kanisani. Wnasema kuwa kwao ilikuwa kama mchezo wa kuigiza kwa sababu walikuwa wakiwaagalia watu wanachofanya na wao kufuatiza, kama ni kusisima na wao walisimama, kama ni kupiga makofi na wao walipiga makofi ili mradi wanafanya kichofanywa pale kanisani. Ukifika muda wa mahubiri hapo iliwawia ngumu sana hadi kufikia kulala usingizi. Lakini sasa tunafurahia kupata mahitji yote tukiwa kanisani kwetu kwa kutumia kutumia Lugha yetu maalum kuanzia matangazo, kwaya na Mahubiri.