Picha Mbalimbali

Karibuni mjionee matukio mbalimbali ya jamii yetu katika picha.

Hapa waonekana wakiwa katika kazi ya kutafsri Biblia ya Lugha ya Alama,
wakijadili jinsi alama zitakavyotumika, kukubalika, kuvutia, na kuonekana

Sehemu ya jamii ya viziwi wa Mkoa wa Kigoma ikiwa na furaha baada ya kupewa DVD ya Biblia ya Lugha ya Alama waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu kwa muda mrefu.

Shaban akifurahi bada ya kupata soda. Hata hivyo, jambo la kusikitisha sana ni kwamba mvulana huyu mwenye umri wa miaka saba, kwa maelezo ya wazazi wake wenyewe hawamjali kwa sababu wanaona kwa ulemavu wa usikivu alio nao hana faida au msaada kwao na hivyo hawako tayari kwa kile walichodai kuingia gharama za kumpatia elimu kwa sababu wao ni masikini.

Kwa yeyote mwenye kuguswa na matatizo aliyo nayo mvulana huyu ili aweze kupata elimu kwa faida yake ya baadaye, awasiliane nasi kwa simu au barua pepe kwa anuani hapo chini

+255757142017 (sms)

info@alamatanzania.com

Hapa Ev. Oscar Mwakampya akiwa na Dada Machozi, mkazi wa Mkoa Kigoma baada ya Kutembelea Kituo cha Mafunzo Stadi kwa Viziwi wakati wa ziara ya kueneza Neno la Mungu mkoani humo.

Matukio

Ukurasa Mkuu

Share

Your encouragement is valuable to us

Your stories help make websites like this possible.